Paroles de la chanson Tukaze Roho par Lava Lava

Chanson manquante pour "Lava Lava" ? Proposer les paroles
Proposer une correction des paroles de "Tukaze Roho"

Paroles de la chanson Tukaze Roho par Lava Lava

Mmmh mmmmh mmmh ;;;
Spice music

Maisha yangu si ya ki papa
Ni vitembele ya nyanya chungu
Dagaa kurusungu, hummh
Niko chakavu na nimechakaa
Yaani naishi ki mungu mungu
Mtetezi wa bunjuu

Mjukuu wa binti simba
Okoa mangala
Wa mwisho kitinda mimba
Mwenye elimu uchwara

Maisha yalivyo nifilimba, akanijalia jallah
Nikaanza kuimba, uniondoke ufukara
Ila bado,
Kipato changu cha chini nacho kina utata
Hata visenti hamsini kuvipata mashaka
Nalia na umasikini mungu ashushe baraka
Enyi wezangu na mimi tusikate tamaa

Tukaze roho, tukaze roho tusichoke
Tukaze roho ,mungu wa kwetu sote
Tukaze roho, eeh  tusichoke
Tukaze roho, mungu wa kwetu sote

Mmh
Japo, maisha yenye ya manati
Hatupati kila tukilenga
Kukicha misumari ya bati
Kuku kapenya kwa tenga

Kula yetu tu ni wasiwasi
Tutapata wapi ya kujenga
Wa kupiga picha masaai
Kulala mbagala kwa chemba

Tunaunga unga mwana (haya ndo mambo yetu)
Hayana tofauti na jana(ndo maisha yetu)
Wazazi kulala na mwana(heey...)
Chumba kimoja mandoo, masufuria (wenyewe tushazoea)

Kipato changu cha chini, nacho kina utata
Ata visenti hamsini kuvipata mashaka
Nalia na umasikini mungu ashushe baraka
Enyi wezangu na mimi tusikate tamaa

Tukaze roho, tukaze roho tusichoke
Tukaze roho, mungu wa kwetu sote
Tukaze roho, eeh  tusichoke
Tukaze roho, mungu wa kwetu sote

Iyo lizer

Wanangu wa bodaboda, tukaze roho
Kina mama vikoba, tukaze roho
Ah rumbesi wabeba virogha, tukaze roho
Vijana wezangu, tukaze roho
Tutapata tu

 

Paroles.net dispose d’un accord de licence de paroles de chansons avec la Société des Editeurs et Auteurs de Musique (SEAM)

Sélection des chansons du moment