Paroles de la chanson Miss u mama par Hanstone

Chanson manquante pour "Hanstone" ? Proposer les paroles
Proposer une correction des paroles de "Miss u mama"

Paroles de la chanson Miss u mama par Hanstone

Ikifika asubuhi mama unaniamsha
Nakuta na chai mezani, umesha chemsha
Kisha, unaweka maji bafuni unanikogesha
Kwani nimekosa nini mpaka unaniacha?

If ungesema mapema,
Kama kesho unaondoka mama
Mwenzio moyo unauma
Na nafsi inasonona

Aah nakukumbuka
Usiku silali nakuwaza wewe
Mpaka najuta kuona umeondoka
Umeniacha mwenyewe

Yalonikuta wala sisemi
Nalia mwenyewe
Mama toka umeondoka

I miss you mama
Mbona umeondoka umeniachia kidonda
I miss you mama
Sili silali mwanao nakonda

I miss you mama
Ila sio siri bado nakupenda
I miss you mama
Haifai mama umeniacha solemba

Mama yangu ungekuwepo singepata taabu
Siku nyingine naumwa nakosa matibabu
Mimi naona Mungu umenipa adhabu
Mpaka hii dunia naiona ya ajabu

Ah, kama chozi lingekurejesha mama
Mimi ningelia usiku na mchana
Mimi naomba Mungu ulale mahali pema
Umetangulia ipo siku tutajaonana mama

Nakukumbuka
Usiku silali nakuwaza wewe
Mpaka najuta mbona umeondoka
Umeniacha mwenyewe

Yalonikuta mama
wala sisemi, nalia mwenyewe
Mama toka umeondoka
Mwenzio bado sijaelewa

I miss you mama
Mbona umeondoka umeniachia kidonda
I miss you mama
Sili silali mwanao nakonda

I miss you mama
Ila sio siri bado nakupenda
I miss you mama
Haifai mama umeniacha solemba

I miss you mama, iye iyee
I miss you mama, iye iyee
I miss you mama, I miss you mama

Nakukumbuka
Usiku silali nakuwaza wewe
Mpaka najuta kuona umeondoka
Umeniacha mwenyewe

Yalonikuta mama wala sisemi
Nalia mwenyewe
Mama toka umeondoka

Paroles.net dispose d’un accord de licence de paroles de chansons avec la Société des Editeurs et Auteurs de Musique (SEAM)

Sélection des chansons du moment