Paroles de la chanson Tusipeane Masifa par Mwana Mtule

Chanson manquante pour "Mwana Mtule" ? Proposer les paroles
Proposer une correction des paroles de "Tusipeane Masifa"

Paroles de la chanson Tusipeane Masifa par Mwana Mtule

Rafiki rafiki yangu
Nina jambo napenda nikueleze
Na kama nitakuudhi nakuomba nisamehe 
Ni jambo kuhusu sifa, usinipe masifa
Mungu ndiye wa masifa tumpe zetu sifa

Rafiki yangu unanishangaza sama
Leo unanisifu kesho unanisengenya
Ah sio vizuri, sio vizuri
Sitaki zako sifa (Sitaki)

Nikikugawia pesa unaniita mfalme
Nikikosa cha kukupea unanitukana mshenzi
Peke yangu no no no sitaki sifa

Tumpe Mungu wetu sifa, tusipeane masifa 
Mungu ndiye wa masifa tusimwibie masifa
Tumpe Mungu wetu sifa, tusipeane masifa 
Mungu ndiye wa masifa tusimwibie masifa
Tumpe Mungu wetu sifa, tusipeane masifa 
Mungu ndiye wa masifa tusimwibie masifa

Hiki kipaji amenigawia Mungu
Usinisifie sana sijajipea mwenyewe
Sio vibaya kunipongeza
Ila usisahau ni Mungu aniniwezesha mimi nafanya vizuri
Sifa na utukufu zimrudie yeye

Na usiniambie mimi ni mhandsome dunia nzima
Utakuwa unanidanganya maana Mungu ameweka mahandsome wengi
Na usimwambie ye ndo mrembo dunia nzima hapana
Hapa kwa dunia Mungu ameweka warembo wengi nani 

Tumpe Mungu wetu sifa, tusipeane masifa 
Mungu ndiye wa masifa tusimwibie masifa
Tumpe Mungu wetu sifa, tusipeane masifa 
Mungu ndiye wa masifa tusimwibie masifa
Tumpe Mungu wetu sifa, tusipeane masifa 
Mungu ndiye wa masifa tusimwibie masifa

Wapo madaktari hosipitalini wanawatibu watu
Sio kwa nguvu zao ni kwa nguvu za Mungu baba
Wapo waandishi wa habari wanatangaza habari
Sio kwa nguvu zao ni kwa nguvu za Mungu baba
Wapo wasanii kama sisi tunapiga mavocal
Sio kwa sababu ya ndimu ni kwa sababu za Mungu baba

Paroles.net dispose d’un accord de licence de paroles de chansons avec la Société des Editeurs et Auteurs de Musique (SEAM)