Paroles de la chanson Wajinga Nyinyi par King Kaka

Chanson manquante pour "King Kaka" ? Proposer les paroles
Proposer une correction des paroles de "Wajinga Nyinyi"

Paroles de la chanson Wajinga Nyinyi par King Kaka

Dear Lord
Today I come before you for two things
Grateful for keeping me alive even though unajua my day
Na kutupea waKenya amnesia
Asante

Sisi ni vipofu na viziwi na tunajua translator wetu alishadedi
2022 already, si mnajua nani ni Prezzi?
Si mnajua nyinyi voters ndio washenzi?
Kwani hamjui mdomo yangu ilibatizwa na wakongwe?
So nashanga akili zenu time ya kura zinajaanga shonde?
Na hiyo wiki ndo najua jirani yangu huwa Mjaka
Kamah kumbe huwanga msapere
Ata salamu hatapata
Piga tu kura na utalala bila kula, a night of tears
Nani skiza na macho na ona with your ears

Swali
Fununu ni ati system ya education ni ya uduu
Is it true? that’s why umepeleka mtoi wako akasome majuu
While graduates wanashika placards kwa traffic
Mtu wa actuarial science anataka kujimada, its so tragic

Swali
Ati Waiguru ako kwa office
Na story ya NYS tulishasahau
Biro moja alibuy 8 thao, Biro tunanunuanga mbao?
Either sisi ndio wajinga ama ako na marking scheme ya accau
Time will tell, Vijana wanabet na Kifo
Wanadai betting imewapea job kuwaliko
City stadium imekuwa renovation for 3 years budget ziwatoshe
While Sonko anadance tu kwa ofe?

Swali
How do you sleep at night knowing mkono yako imeua? Not close to purity
Wordsmith King Kaka arrested for fighting impunity
Ata wakijam na hatupati bread hawatusomi na Sikwani
Promises hamuweki Hii ni relationship ya aina gani
Is it true?
Uko na account offshore zimejaa money
Na account ya daughter ya Waititu iko na depo ya 100 mita
Ukipelekwa kotini ni escort ya polisi kama sita

Ladies and gentlemen official speech by mbwa mwitu
Wacha avae ngovi ya kondoo kwanza ndio tumsifu
Si basi wakam kwa church watoe pesa tulitoa kama tax
Na pastor anakiss ass, ampatie hadi asome kaVerse
Na sisi tuko busy wajinga nyinyi tuna clap

Wakinisnipe tonight si mnajua ni kwa nini
Nitakufia watu mi siogopi mimi
Wasijifanye hapo watalost na ata chuma u rust
Na hizo ganji hamtazikwa nazo news flash
Flesh urudi kwa dust
Nchi inaongozwa na thieves
Na ukiogopa jua hauwezi kuwa chief
Iba hizo mamita mmh-scott free, niibe tu kuku ntalala ndani
Atleast pastor Ng’ang’a ana washinda anadanganyanga adharani

Hapo parliament kwani mnashda gani
Si mtuibie Kiplani
Mmetumiwa shetani gani na job ziko wapi?
Swali, Ni ukweli lazima uretire ndio upate job
So inamaanisha lazima kwanza nipatie job, ndio nipate job job?

The youth ni moody at 90 na Gikonyo at 80
Manifesto mlisema job ni plenty
KQ wali samehewa deni ya 24 billy, sugar milly, farms ni 40 billy
Na ujinga yenu mnaweka students hawajalipa kwa gazeti HELB
Wajinga Nyinyi!

Hizo mlango zenu vile mmebeef security, hamuwezi nikubalia hodi
Remember me, my mom anaitwa Wanjiku na my father is a nobody
Naskia mafuta imepanda tena
Inatoka Turkana ndio irudi tena
Hesabu ya 1 plus 1 inawachenga
Mtaenda retreat kuidiscuss tena?
Na mjiongeze pesa ya tax payer tena?

Laptop ni multi billion project, na walimu ushago hawana lights
Wanacharge kwa generator shopping center, its not right
Wasipandishe tax, hizo ndio dreams mi uwa nazo nikituna
What are we really doing as a country saa zile tunachuja Miguna?
Petroli imepanda so inamaanisha polisi wata operate kama customer care
Busaa na chwara zinamaliza mayout
Enyewe Stivo was right, mihadarati haiwezi
Wachane na polisi wafanye raid tena
Ama ni vile OCS hajapewa yake na kila mwizi
Oh, i mean ya kila mwezi
Na polisi wako in cahoots, hao ndio uSupply wagondi na guns za ku shoot

Swali
Kazi ni formalities tu, na uki apply ina bounce
Ni ukweli KPLC wanatuwekea bills haziko kwao, na zinaenda kwa personal accounts
Welcome to our country where politician wana ujinga za kila aina
Economy imekuwa hard, hakuna kitu ya kuteremsha chai na
Karibu to the Kenya Republic of China
I support teachers, doctors wakistrike
Na the president is saying ati kama hawarudi watachujwa
Hakuna siri kwa nyumba, naskia jirani bibi anakula you know what i mean
Police anaishi kwa keja zimeseperatiwa na curtains, i mean in 2019?
Na hizo damu zitawafuata to the coffin

Punda idedi lakini mzigo ifike
KCSE hazijafika sababu ya floods so instead wacha niulize maswali
Harambee stars wanalala kwa floor airport flani
While mnahire private jets?

Swali
Disaster mnakimbia kusema vile mtacreate enquiry
Is it true, women rep ndio wanadishi pesa ya pads meant for girls?
Maize scandal, wako na matusi kwa national TV, such role models
Youth unemployment
Politicians ni addicts wa pesa
KRA wanatuibia ndio wapatie wezi pesa
Deadline ya tax return ni Tuesday
Jengeni tu, sips tea iko na mercury kwa shuge

Swali
Is it true war iko funded as tunaloose KDF soldiers daily so unalia?
Ndio maana tumeshindwa kutoa troops Somalia
Mnakula pesa ya health ndio maana mkenya hawezi afford
The moment you fall sick tunaskia unapata treatment abroad
Na voter akidedi na Cancer, Kera
Perfect opportunity atoe coffin na transport, on top auze sera
Hapo ndio mras uwasha kiLucy
In the name of treatment kuna power ni Kirusi
Moha umefunga jicho, jicho pevu ni kipofu
Huduma number kumbe ilikuwa u ka scam flani?
Na Maraga anataka magari

Rais unawaona hapo ni wanajeshi waNavy wakionyesha umaarufu wao wa vita ya kulinda nchi wakiwa kwa maji
Wajinga Nyinyi
While Mariam na daughter wake hajapatikana wiki mbili
Wako kwa maji
Sema MCSK Kutuibia
Kwa traffic uko on the wrong side ndio urush kutuibia
5 years ndio zinaisha naskia umeanza kurudi kwa ground
Wacha kupretend and all Kenyans know kwa ground vitu ni

Swali
Sijui ka unakumbuka mimi ndio nilikuweka hapo
Can’t see you nikaa tunacheza tapo

Swali
Ama na assume ni vile ulibuy simu uko na line mpya
Na haushikangi numbers haujui
I stopped being your friend unanitreat namna ya adui

Swali
Stadium ziko wapi? Kazi ziko wapi?
Ile manifesto iliniwow iko wapi?
Na hii handshake kwani ni ile sisi ufinya Kenyatta kwa mkono ya karao?

Swali
Ata kama tuko na Kenyatta, ndio maana i strongly feel hatujapata Uhuru!

Paroles.net dispose d’un accord de licence de paroles de chansons avec la Société des Editeurs et Auteurs de Musique (SEAM)