Paroles de la chanson Ayiola par Harmonize

Chanson manquante pour "Harmonize" ? Proposer les paroles
Proposer une correction des paroles de "Ayiola"

Paroles de la chanson Ayiola par Harmonize

Nilifundishwa na Bibi kijijini jinsi ya kupenda
Na mwanamke hapigwi
Na ngumi ila upande wa kanga
Tena mapenzi sio league
Nikakubali kushindwa
Mi sikufunzwa graji
Tushindane risasi kwa panga

Mbona niliku thamini
Mengi nikakusevia
Sitosema hadharani wengi wakayasikia
Sio wakunipanda kichwani
Hukumbuki tuliko tokea
Na kunishusha thamani
Kipi nilicho kosea


Ingawa kidogo nlichopata
Nkajinyima uridhike
Ila hukujali ukanikatili moyoooo!
Majirani walinicheka ulipo ni force nipikee
Aaaahh! Sio siri ilinivunja moyoo

Kisirani ugomvi bila chanzo
Ni ukweli uko moyoni
Sina budi nilivue pendo
Ingawa Kishingo upande
Aiyoo aiyola eeeh!
Sito force unipende
OoohKishingo upande
Aiyoo aiyola eeeh!
Basi bora uendee

Sitosema mapenzi basi nimeumbwa na moyo
Moyo wenye matamanio na unapenda pia

Ila nitaijutia nafsi nilikufanya chaguo
Aaah! Chaguo la moyo kumbe ulipita njiaa

Nilivo wanyima ndugu
Visiri nikakutunzia
Usijee leta vurugu akili ukaitibuaa
Najuta Kujitia bubuu
Sitaki vya kusikia
Kisa pendo unisurubu
Mengi nishafumbia

Mbona niliku thamini
Mengi nikakusevia
Sitosema hadharani wengi wakayasikia
Sio wakunipanda kichwani
Hukumbuki tuliko tokea
Na kunishusha thamani
Kipi nilicho kosea


Kisirani ugomvi bila chanzo
Ni ukweli uko moyoni
Sina budi nilivue pendo
Ingawa Kishingo upande
Aiyoo aiyola eeeh!
Sito force unipende
Oooh baki Kishingo upande
Aiyoo aiyola eeeh!
Basi bora uendee

Kishingo upande kishingo upande
Aaaah
Na maximize oooh am nice baibe, am nice baibe

Paroles.net dispose d’un accord de licence de paroles de chansons avec la Société des Editeurs et Auteurs de Musique (SEAM)

Sélection des chansons du moment