Paroles de la chanson Msumari par Diamond Platnumz

Chanson manquante pour "Diamond Platnumz" ? Proposer les paroles
Proposer une correction des paroles de "Msumari"

Paroles de la chanson Msumari par Diamond Platnumz

Ay-Ayo, Trone
Mmmh

Ni utoto tu, ila mie kwako sipindui
Ndio maana usiku nikinuna, najichekesha asubuhi
Ni ujinga tu, ila mie kwako fala
Ndio maana usipo pokea simu, siwezagi lala
Mmm, umenifunza tofauti ya kupenda na kupendana
Na kuongea sio sauti hata macho husemezana
Na mapenzi yanataka, 'imara, kuaminiana
Nami kwako sina shaka, 'ewawa, utachofanya

Na hivi vi inzi, vya kuzengea wizi, vikija anga hizi, visikunyime amani
Lala usingizi, upepo barizi, mie mambo ya uzinzi, 'aku!, vya kazi gani, baby?

Hapo hapo ilipo mbao (Gongelea na msumari)
Oh, penzi letu tuboreshe, (Gongelea na msumari)
Ezeka na bati, honey (Gongelea na msumari)
Mvua ya chuki isipenyeshwe (Gongelea na msumari)
Mm, mm-m

Oh, njiwa nenda, njiwa, 'njiwa peleka salamu (Peleka salamu)
Naivasha, Kivule, 'Mombasa zifike Lamu
Njiwa nenda, njiwa, 'njiwa peleka salamu, ziende mpaka kwa yule, 'lonitesa mwanaharamu
Si alisema mimi, sitopata wa thamani, asa hii ni nini?
Umuulize huyu nani, wamebaki kutabiri si punde tutaachana
Wambie sio kwa penzi hili, mbona wataroga sana

Na hivi vi inzi, vya kuzengea wizi, vikija anga hizi, visikunyime amani
Lala usingizi, upepo barizi, mie mambo ya uzinzi, 'aku!, vya kazi gani, baby?

Hapo hapo ilipo mbao (Gongelea na msumari)
Oh, penzi letu tuboreshe, darling (Gongelea na msumari)
Ezeka na bati, honey, oh (Gongelea na msumari)
Mvua ya chuki isipenyeshwe (Gongelea na msumari)
Mmm

Wasafi

Paroles.net dispose d’un accord de licence de paroles de chansons avec la Société des Editeurs et Auteurs de Musique (SEAM)

Sélection des chansons du moment