Paroles de la chanson Bwana Utetenao par Christina Shusho

Chanson manquante pour "Christina Shusho" ? Proposer les paroles
Proposer une correction des paroles de "Bwana Utetenao"

Paroles de la chanson Bwana Utetenao par Christina Shusho

Ee Bwana utete nao wanaoteta nami, upigane nao wanaopigana nami,
Ee Bwana utete nao wanaoteta nami, upigane nao wanaopigana nami
Uishike ngao na kigao usimame unisaidie,
Uutoe mkuki uwapige ooh wanaonifuatia,
Uambie nafsi yangu mimi ni wokovu wako,
Uutoe mkuki uwapige ooh wanaonifuatia,
Uambie nafsi yangu mimi ni wokovu wako,
Wananiuliza mambo nisiyoyajua,

Ee bwana utete nao wanaoteta nami,
(Bwana pigana nao) upigane nao(pigana nao) wanaopigana nami (naomba
Wee nitetee) ee bwana utete nao (nitetee)wanaoteta
Nami(Baba nitetee) upigane nao (pigana nao)wanaopigana nami

(Eehh)

(Waaibishwe, wafedheheshwe, warudishwe nyuma wanaotafuta nafsi yangu,
Wafadhaishwe, wawe kama makapi,
Mbele ya upepo, malaika wa bwana waangushe chini)

Wananilipa mabaya, badala ya mema,
Kutwa kucha waniwinda, ili niteseke,
Kiganjani mwako niweke (ee Mungu wangu) ubafuni mwako
Nikumbatie (Jehova wangu), mikononi mwako uniweke (ee Mungu wangu)
Ubafuni mwako nikumbatie, (Jehova wangu),
Eehh

Ee Bwana utete nao wanaoteta nami,
(Bwana pigana nao)upigane nao (pigana
Nao) wanaopigana nami (naomba wee nitetee)
Ee Bwana utete nao (unitetee) wanoteta nami,
(Baba nitetee) upigane nao (pigana nao) wanaopigana nami,

Njia yao iwe giza na utelezi, malaika wa Bwana, akiwafuatia,
Uharibifu wapate kwa ghafula,
Waharibifu waanguke ndani yake
Mimi bure wasinisimange bure wasinigonge,
Na wovu wao aloficha wamnase mwenyewe,
Ila sababu wamenichimbia shimo la hasira,
Mifupa yangu, wataitazama, Bwana ni nani,
Aliye kama wewe, na nafsi yangu, itamfurahia Bwana,

{Wapendeza Bwana wapendeza,
Ee Bwana wapendeza, katika hili najua utatenda aah
Nitetee Bwana nitetee,
Ee bwana nitetee, katika hili najua utatenda aah}

By; Driverjoseph

Paroles.net dispose d’un accord de licence de paroles de chansons avec la Société des Editeurs et Auteurs de Musique (SEAM)

Sélection des chansons du moment