Paroles de la chanson Nyumba ya Milele par 20 Percent

Chanson manquante pour "20 Percent" ? Proposer les paroles
Proposer une correction des paroles de "Nyumba ya Milele"

Paroles de la chanson Nyumba ya Milele par 20 Percent

Wengine wananipenda, baadhi wananiponda
Wengine wananisifia, wengine wananipondea
Sitoweza kuwatenga, sitoweza kuwatenga
Hata kama wakiponda daima nitawapenda

Wanaona nawabana, wao kuwa nayafanya
Hali hii itakuwaje mi nitapoiaga dunia

Wengi watalia, wengine watafurahia
Siku itakapofikia mi utappoiaga dunia
Wengi watalia, wengine watafurahia
Siku itakapofikia mi nitapoiaga dunia

Kwani kufa kufaana
Na wengine kifo waaniombea
Kwani kufa kufaana
Na wengine kifo wanakuombea

Nikifikiria kifo, kulala siwezi
Sihitaji mpenzi na sifanyi ushenzi
Nahitaji nikae tu, nimuombee Mwenyezi
Siku ya kifo changu anipende mama kafi

Ukimaliza kuteseka unakwenda kule
Ile ndio nyumba ya milele
Haina hodi hodi, haina kodi kodi

Ukimaliza kuteseka unakwenda kule
Ile ndio nyumba ya milele
Haina hodi hodi, haina kodi kodi

Maisha ni kutoka kisha kucheka
Yaani ukishafika juu ni kudondoka
Umepita kwenye raha shida ni balaa
Pumzi umeshakata ndo unapanda motokaa

Mpende mama mtenge baba ndicho umejenga
The way utacholipwa ndicho umetenda
Tuko up tuko down muda unakwenda
Tupo njia ya Kanumba na Papa Wemba

Dada mama, baba unanitenga
Zikifika nitaondoka bila kupenda
Unapojenga ukipenda funga renta
Nitazima ka mshumaa kisha nakwenda

Naona kunadondoka pigwa panga
Chini hakuna godoro kuna michanga
Mida ya kula modoo kufunga kanga
Sasa legeza kidogo funga kamba
Sitaki tena midoo nataka mwanga
Upepo sina maji sina nipe sanda

Ukimaliza kuteseka unakwenda kule
Ile ndio nyumba ya milele
Haina hodi hodi, haina kodi kodi

Ukimaliza kuteseka unakwenda kule
Ile ndio nyumba ya milele
Haina hodi hodi, haina kodi kodi

Paroles.net dispose d’un accord de licence de paroles de chansons avec la Société des Editeurs et Auteurs de Musique (SEAM)

Sélection des chansons du moment