Paroles de la chanson Kasuku par Eric Omondi

Chanson manquante pour "Eric Omondi" ? Proposer les paroles
Proposer une correction des paroles de "Kasuku"

Paroles de la chanson Kasuku par Eric Omondi

Mmmh 
Kasuku kwenye sauti ya porojo
Misusing ma doh na mahongo
Tunapambana na hali
Doh Fuliza tuma mkopo
Prado na suti pesa wakila tu solo

Mmmh wakiteremsha na pombe pombe
Na matuzo wajipe sifa
Na walivyo watundu kujionyesha, mabarobaro
Siwapi kura tena kamwe

Tukoroge sumu kwenye sukari ya Mexico
Tunakunywa sewer Kenya tupate kwashiakor
Tena wavimbe na vitambi, Turkana wafa njaa
Jasho letu mwamumunya mmetufika koo

Na Tena, likizo Dubai, tamuu
Kujiongeza hela, tamuu
Kuhepa hatia, tamuu
Tamu tosheka

Sie tukikufa njaa hamuu
Tukisaka kamtego hamuu
Mwafanya tutoane damuu
Damuu ju yao

Nyie kuiba waziwazi twawaona
Matajiri filthy na madola dola ka mchele
Taabu, tunakosa kazi waloahidi
Ufisadi zaidi, watupwe pia kwa Celli

Waambie mafinje finje sio gharama ya maisha
Tushawasoma sana, sa sisi tushawachanuka
Waambie sisi werevu sio jogoo la pasaka
Wanajisumbua kurekebisha sisi tumeshawachoka

I still wonder, mimi ninakumbuka, 2007-7
Tulivyomwaga yetu damu, na machozi tele
Tena bila haya, wazi wanaonyesha maovu ovu
Hawadai kuacha hivyo viti

Kwa kukuwa
Tukoroge sumu kwenye sukari ya Mexico
Tunakunywa sewer Kenya tupate kwashiakor
Tena wavimbe na vitambi, Turkana wafa njaa
Jasho letu mwamumunya mmetufika koo

Na tena, likizo Dubai, tamuu
Kujiongeza hela, tamuu
Kuhepa hatia, tamuu
Tamu tosheka

Sie tukikufa njaa hamuu
Tukisaka kamtego hamuu
Mwafanya tutoane damuu
Damuu ju yao

Ebo, bila haya wanarudi kusimama tena
Watazame, kusimama tena
Tunawashangaa, kusimama tena
Yaani Te, tuwateme

Paroles.net dispose d’un accord de licence de paroles de chansons avec la Société des Editeurs et Auteurs de Musique (SEAM)

Sélection des chansons du moment