Paroles de la chanson Utatulia par Lava Lava

Chanson manquante pour "Lava Lava" ? Proposer les paroles
Proposer une correction des paroles de "Utatulia"

Paroles de la chanson Utatulia par Lava Lava

Kiangazi masika ukiichanganya
Vyote vikashuka kwangu vitanielemea
Ntakosa pa kushika ntavavanya
Wewe ndo mwandani wangu nliokuzoea
Ntunza vyangu visiri mwenye kunisitiri
Fundi mitambo
Kinga yangu ya mwili usiyelipa bili
Kuchoma changu
Simtaki kafiri jangiri mwingi wa mambo
Moyo akaukatilli
Nikondeshe mwili
Ajifanye rambo

Si unajua
Dalili ya mvua mawingu
Ikitaka kunyesha
Huwa yanatanda
Nami si unanjua aah
Nimeumbwa na wivu
Kidogo tu presha
Yanshuka yapanda
Niahidi kama

Utatulia aaah Baby
Niahidi kama (utatulia aaah)
Hhhmm nisibaki nkashika tama
Utatulia aaah Baby
Niahidi kama (utatulia aaah)
Hhhmm wasiniibie cha ngama

Maneno yangu
Si biblia wala masaafu
Useme usibadili hhhmm
Jichunge kipenzi changu
Unanisikia usicheze rafu
Yatimie waliotabiri
Yeah yeah…
Usijifanye ronaldinho
Penzi utie mbwembwe utahaaribu
Visokolokwinyo wakupitie denge kukujaribu
Kina capachino wakakutia wenge kwa vizabibu
Wakugongeshe mvinyo
Ukaota mapembe iwe aibu

Si unajua
Dalili ya mvua mawingu
Ikitaka kunyesha
Huwa yanatanda
Nami si unanjua aah
Nimeumbwa na wivu
Kidogo tu presha
Yanishuka yapanda
Niahidi kama

Utatulia aaah Baby
Niahidi kama (utatulia aaah)
Hhhmm nisibaki nkashika tama
Utatulia aaah Baby
Niahidi kama (utatulia aaah)
Hhhmm wasiniibie cha ngama

Eeeh eh Yani kama (ukitulia tulia)
Sitathubutu macho kupepesa (Ukitulia tulia)
Ukinipa kiduchu nitatosheka (Kama ukitulia tulia)
Sitofwata nguruchu niende teseka (Ukitulia tulia)
Eeeh Nami ntatulia

 

Paroles.net dispose d’un accord de licence de paroles de chansons avec la Société des Editeurs et Auteurs de Musique (SEAM)

Sélection des chansons du moment