Paroles de la chanson Utashangaa par Guardian Angel

Chanson manquante pour "Guardian Angel" ? Proposer les paroles
Proposer une correction des paroles de "Utashangaa"

Paroles de la chanson Utashangaa par Guardian Angel

Hesabu baraka zako moja kwa moja
Zipe majina, zipe majina
Hesabu baraka zako moja kwa moja
Na utashangaa yale Mungu ametenda

Na utashangaa, na utashangaa
Na utashangaa, wewe utashangaa
Na utashangaa, na utashangaa
Na utashangaa, wewe utashangaa yale Mungu ametenda

Kumbuka ulipokuwa umelazwa
Wakakata tamaa
Wakatuma ujumbe kwa wote
Marafiki jamaa

Wakasema huyo ametuacha
Yamebaki masaa
Ona sasa ulivyo na afya nzuri
Bwana ametenda

Umeiona siku ya leo, Bwana ametenda
Familia uliyo nayo, Bwana amekupa
Hata nguo ulizo nazo, Bwana amekupa
Oooh we utashangaa yale Mungu ametenda

Hesabu baraka zako moja kwa moja
Zipe majina, zipe majina
Hesabu baraka zako moja kwa moja
Na utashangaa yale Mungu ametenda

Na utashangaa, na utashangaa
Na utashangaa, wewe utashangaa
Na utashangaa, na utashangaa
Na utashangaa, wewe utashangaa yale Mungu ametenda

Yesu ana mikate mitano na samaki wawili
Na kuna watu elfu tano wake pia watoto
Neno lasema alishukuru na vikaongezeka
Watu wakala na vikabaki vinashangaa

Jifunze kumshukuru Bwana
Kwa hicho ulicho nacho
Hata kama ni kidogo sana 
We shukuru unacho

Kuna yule anayetamani
Kuwa hapo ulipo
Wewe utashangaa 
Yale Mungu ametenda

Hesabu baraka zako moja kwa moja
Zipe majina, zipe majina
Hesabu baraka zako moja kwa moja
Na utashangaa yale Mungu ametenda

Na utashangaa, na utashangaa
Na utashangaa, wewe utashangaa
Na utashangaa, na utashangaa
Na utashangaa, wewe utashangaa yale Mungu ametenda

Paroles.net dispose d’un accord de licence de paroles de chansons avec la Société des Editeurs et Auteurs de Musique (SEAM)

Sélection des chansons du moment